Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwa tayari kuzuia maandamano hayo.
|
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maanadamano hayo |
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwakamata baadhi ya wanafunzi wakati wa maanadamano hayo. |
| Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakimkamata mmoja wa wanafunzi wakati wa maanadamano hayo, ambapo walimkamata na kkumuweka kwenye gari la polisi. |
skari wengine wakiwakimbiza wanafunzi ili kuwakamata |
| Akari wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) mkoa wa Simiyu wakiwa katika eneo la shule ya sekondari Bariadi, kuhakikisha wanafunzi wanaingia madarasani ili wasiendeleze maandamano. |
| wanafunzi hao wakiwa wanaandamana, barabara kuu ya bariadi-lamadi |
ZAIDI ya Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari ya Bariadi halmashauri
ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga barabara kuu
ya Bariadi –Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Deus Toga.
Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya
mkurugenzi wa halmashauri,lakini ilishindikana baada ya kikosi cha
jeshi la polisi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.
Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana pia baada ya askari hao kuwazuia tena eneo la Hospitali teule ya mkoa (somanda).
Baada ya hali hiyo wanafunzi hao ambao ni kidato cha kwanza hadi cha sita waliamua kukaa katikati ya barabara huku wakimba nyimbo za kushinikiza kuwa hawamtaki mwalimu Paul Lutema ambaye alikuwa amepelekwa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
“hatumtaki mwalimu Lutema……tunamtaka mwalimu wetu Toga…..hatumtaki
Lutema……Tunamtaka mwalimu Toga”
Wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kumkataa mwalimu Lutema na kumtaka mwalimu Deus Toga wanafunzi hao walianza kuwarushia mawe askari hao wakitaka wasiwazuie kwenda kofisi ya mkuu wa mkoa.
Baada ya hali hiyo jeshi la polisi walianza kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao huku wakiwafukuza kurejea katika eneo la shule ambapo baadhi yao walikamatwa na kupigwa virungu na kuwekwa ndani ya magari ya polisi hadi kupelekwa kituo cha polisi Bariadi.
“toka mwalimu huyu kafika shuleni hapa ufauru umeongezeka na
migogoro ya shule iliyokuwepo haipo tena,na duka la shule lilikuwa limefungwa
kutokana na migogoro ya walimu lakini toka amekuja hiyo migogoro imekwisha na
duka linafanya kazi’’Alisema Justine Mshana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni