Jumatatu, 13 Machi 2017
Alhamisi, 9 Machi 2017
Jumatano, 8 Machi 2017
Rais Magufuli na mkewe wawasili mkoani Dodoma
Rais
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amewasili Mkoani Dodoma
ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa, Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano
Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi.
Mhe. Dkt. Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ataongoza kikao na mikutano hiyo kuanzia tarehe 10 - 12 Machi, 2017 Mjini Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli waliwasili
jana katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma akitokea Mkoani Morogoro
ambako jana tarehe 06 Machi, 2017 alizindua uwanja wa kisasa wa
ndegevita wa Ngerengere.
SAA MBILI ZA MAANDAMANO WANAFUNZI BARIADI, Zilivyo simamisha mji wa Bariadi.
Mama Mlezi wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Afariki Dunia
Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo.
Kupitia
mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru jamii kwa
salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko nyumbani kwa
marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko yatakuwa
Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri.
"Mama
amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee
Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. Mama
yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani
Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo". Kauli ya
Jakaya Kikwete
Naye
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu
ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya
leo.
"Ndugu
na marafiki nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha Bibi yetu Bi. Nuru
Khalfan Kikwete kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili
alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana" Amesema Ridhiwan Kikwete.
Ndugu wapendwa, nawashukuru sana kwa salamu za pole na upendo kufuatia
kifo cha Mama yangu mdogo mpendwa Bi Nuru binti Halfani Shomvi. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. – JK— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama yetu mdogo aliitwa jana na Mola, na kuitika. Shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mazishi yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
CUF ya Maalim Seif kuiburuza CUF ya Prof.Lipumba mahakamani
Bodi
ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF ), imefungua kesi ya madai
dhidi ya wanachama wake nane akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya
Kesi
hiyo imefunguliwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitaka
wanachama hao wasijihusishe na harakati zozote za chama hicho.
Mbali
ya Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua mkoani Tabora, wadaiwa wengine
ni Thomas Malima, mbunge wa Mtwara Mjini,Mafta Nachumu, Omar Mhina
Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.
Maombi
hayo mbayo yametajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri
yamewasilishwa na Wakili wa bodi, Hashim Mziray na yamepangwa
kusikilizwa kesho.
Katika
maombi hayo yaliyopewa namba 1 ya mwaka 2017, bodi inaiomba mahakama
kutoa zuio kwa wadaiwa kutojihusisha katika masuala yeyote yanayohusiana
na chama hicho.
Mbali
ya maombi hayo, pia Wakili Mziray amewasilisha maombi madogo ya kuiomba
mahakama kuwaamuru wadaiwa wasijihusishe na mikutano ya chama hicho.
Aidha,
Mziray aliomba maombi yao madogo yasikilizwe kwa upande mmoja wa wadai
tu kwa kuwa wamechelewa kuwapatia nyaraka za madai yao wadaiwa.
"Mheshimiwa
tunaomba tusikilizwe upande mmoja ukizingatia maombi yameletwa chini ya
hati ya dharula na kwa mujibu wa sheria mahakama hii... inayo mamlaka
ya kufanya hivyo".
Hakimu Mashauri alisema anakubaliana na upande wa wadai na maombi hayo yatasikilizwa kesho mahakamani hapo.
Hatua
ya Bodi ya CUF, kukimbilia mahakamani inakuja ikiwa ni siku moja baada
ya upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif
Shariff Hammad kupinga uteuzi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa
Ibrahim Lipumba.
Uteuzi
wa Profesa Lipumba ambao unapingwa ni ule alioufanya Machi 6, mwaka huu
baada kuwaondoa katika nafasi zao, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi,
Omar Ali Shehe.
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim Abdull Bimani, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Abdullah Bakar Hassan.
Wengine
ni Pavu Juma, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadam na Sheria, Mahmoud
Ali Mahindo na Katibu wa Jumuiya ya Vijana, Yusuph Salim.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






















